Jumamosi 6 Juni 2026 - 23:00
Baraka za Ayatullah Fayyadh ndani ya Hawza ya Najaf hazitasahaulika

Hawza/ Ayatullah Makarim Shirazi ametuma salamu za rambirambi kufuatia kufariki kwa Ayatullah Hajj Sheikh Ishaq Fayyadh, mmoja wa Mar'ajii wakubwa wa Taqlid wa Najaf.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa rambirambi wa Ayatullah Makarim Shirazi ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Habari ya kufariki mwanazuoni wa Rabbani na Marjii mtukufu, Ayatullah Hajj Sheikh Ishaq Fayyadh (Mwenyezi Mungu aitakase sehemu yake ya mapumziko), imesababisha huzuni na masikitiko makubwa na imeitumbukiza Hawza Tukufu ya Najaf Ashraf katika maombolezo.

Miaka mingi ya uwepo wake mjini Najaf, kulea wanafunzi wengi, kuandika vitabu, kusimamia na kuwa na uelewa wa kina wa mwelekeo wa kielimu wa Hawza hiyo, pamoja na kuwaongoza Waumini na wafuasi wake wa Taqlid, ni sehemu tu ya baraka za uwepo wa faqihi huyu ambae hatasahaulika, na athari zake njema zitaendelea kubaki, Inshaallah.

Mimi ninatoa pole kwa msiba huu mchungu kwa Hawza ya Najaf Ashraf, mataifa ya Waumini wa Afghanistan na Iraq, kwa wafuasi wote na wapenzi wa Marjii huyu aliyefariki, na hasa familia yake tukufu. Pia namwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe marehemu huyo mwenye sa'ada daraja za juu na amfufue pamoja na mawalii wa Mwenyezi Mungu, na awape waliobaki subira njema na malipo makubwa.

Na amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka Zake

Qum – N'asser Makarim Shirazi
16/3/1405 H.Sh / 6 June 2026

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha